Wakufunzi wa Jeshi la Russia 100 wawasili Niger kutoa mafunzo kwa wanajeshi

  • | VOA Swahili
    1,246 views
    Televisheni ya taifa ya Niger inaripoti kuwa wakufunzi wa jeshi la Russia mia moja wamewasili katika taifa la Sahel kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake jinsi ya kutumia vifaa vya kijeshi vipya vilivyotolewa na Russia. Vifaa hivyo na wakufunzi hao wamewasili kwa ndege ya mizigo Ilyushin -76 Jumatano jioni. Ujumbe uliopachikwa katika mtandao wa kijamii wa televisheni ya taifa umesema vifaa hivyo mfumo wa ulinzi wa kujihami na mashambulizi ya angani. - AP #russia #niger #wagner #military #voa