Wakulima katika kaunti ya Nyandarwa watakiwa kupanda mimea ya kustahimili ukavu

  • | Citizen TV
    81 views

    Wakulima katika eneo bunge la Ndaragua kaunti ya Nyandarwa wamehimizwa kupanda mimea inayostahimili kiangazi na kukomaa mapema ili kujikinga wakati wa ukame. Wito huu ulitolewa wakati wa mkutano uliowaleta pamoja wakulima wa eneo hilo. Viongozi wa eneo hilo walikariri haja ya upanzi huu, kuepuka athari zilizoshuhudiwa wakati wa kiangazi cha muda mrefu. Ni hali ambayo iliwalazimu wakaazi wengi katika eneo hilo kutegemea chakula cha msaada na kusababisha baadhi ya wanafunzi kuwacha masomo. Kwenye kikao hicho, wakulima pia walitakiwa kuimarisha uhifadhi wa maji.