Skip to main content
Skip to main content

Wakulima kote nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia pembejeo zilizothibitishwa na mamlaka husika

  • | Citizen TV
    141 views
    Duration: 1:46
    Wakulima kote nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia pembejeo zilizothibitishwa na mamlaka husika za ubora ili kuepuka hasara katika msimu huu wa upanzi. Onyo hili linajiri wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la pembejeo ghushi sokoni, hali inayotishia uzalishaji na usalama wa chakula nchini. Wakizungumza katika uwanja wa Kitale Club, kaunti ya Trans Nzoia, baada ya kuandaa mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na Kenya Seed kwa lengo la kuhamasisha wakulima, wataalamu wa kilimo walisisitiza umuhimu wa kununua mbegu, mbolea na dawa kutoka kwa wauzaji walioidhinishwa pekee. Wanasema kuwa matumizi ya pembejeo bandia husababisha mazao duni, upotevu wa fedha na kudorora kwa uchumi wa mkulima.