Wakulima kutoka Siaya wafunzwa upanzi wa miembe na shirika la KEPHIS

  • | Citizen TV
    265 views

    Kaunti ya Siaya inazalisha zaidi ya miche elfu 40 ya miembe kila msimu. Wakulima 57 wanaomiliki maeneo ya kukuza miche ya miembe ya kupandikiza wanapokea mafunzo kuhusu kilimo hicho kutoka kwa shirika la afya ya mimea nchini, KEPHIS. Aidha wakulima 7 wamepokea vifaa maalum vya kukinga mimea yao.