Wakulima Navakholo washauriwa na Kamishna wa Magharibi ya kenya Macharia kutouza mahindi mabichi

  • | Citizen TV
    144 views

    Kamishna wa eneo la Magharibi ya kenya Irungu Macharia, amewashauri baadhi ya wakulima wanaouza mahindi yao yakiwa mabichi mashambani kwa bei duni. Kulingana naye, hatua hiyo itachangia upungufu wa chakula wakati wa mavuno ya mahindi yakikauka. Akitoa hotuba kwa wakaazi wa kaunti ndogo ya navakaholo, Macharia ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha baadhi ya wakulima kuuza mahindi shambani wakati taifa linakabiliwa na gharama ya juu ya maisha. Kamishna wa Kaunti Ndogo ya Navakaholo, Joseph Sadia, naye anasema kwamba wakulima hao wananyanyaswa na mawakala wanaonunua mahindi hayo kwa bei ya chini mashambani.