Wakulima wa kahawa nchini wamehimizwa kutopanda mibuni maeneo yaliyokuwa na misitu, kama njia ya kuwahakikishia soko la bidhaa hiyo ulaya, kufuatia kanuni za ununuzi wa kahawa zilizopitishwa na muungano wa mataifa ya EU.
Ombi hili limetolewa na muungano wa wakulima wa kahawa wa New KPCU ulioongoza shughuli ya usambazaji wa miche ya kahawa ya kisasa kwa wakulima eneo la Mukurwe-ini kaunti ya Nyeri, baada ya serikali kukamilisha zoezi la usajili wa wakulima wa mmea huu na maeneo ambayo wanailima kahawa yao