Wakulima wa mpunga Mwea watumia teknolojia ya ratoon kuongeza mavuno mara mbili

  • | Citizen TV
    156 views

    Wakulima wa mpunga katika eneo la Mwea katika Kaunti ya Kirinyaga wanatumia teknolojia mpya ya kilimo ili kuongeza mavuno. Teknolojia inayofahamika kama ratoon inawawezesha kuvuna kwa awamu mbili kutokana na mimea iliyopandwa mara moja. Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo nchini, KALRO limefanya utafiti na kubuni mbinu hii ili kuziba pengo la uzalishaji wa mpunga, kando na kukithi mahitaji yanayozidi kuongezeka nchini.