Wakulima wa Mwea na Ahero wapinga uamuzi wa kuagiza mchele kutoka Nje, wazua wasiwasi sokoni

  • | Citizen TV
    252 views

    Wakulima wa mpunga maeneo ya Mwea na Ahero sasa wanasema Kenya ina mazao ya kutosha, ikipinga uamuzi wa serikali wa kuagiza tani laki tano za mchele kutoka mataifa ya kigeni. Wakulima hawa wakiishutumu serikali kwa kukosa kuwahusisha katika uamuzi huo ambao walisema utawaacha njia panda kutokana na ukosefu wa soko la mazao yao. Hata hivyo, wizara ya kilimo imesema kuwa uamuzi huo uliafikiwa kutokana na upungufu wa mchele uliosababishwa na kubadilika kwa misimu ya mvua