- 161 viewsDuration: 2:23Wakulima kaunti ya Kilifi wamefunzwa mbinu za kuendeleza kilimo katika sehemu kame ili kukabili changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Kulingana na wakulima hao, hatua hiyo itawasaidia kuboresha kilimo hasa nyakati za kiangazi. Aidha wataalam waliotoa mafunzo hayo wameitaka serikali kutoa elimu endelevu Kwa wakulima kote nchini ili kufaulu kutimiza lengo la utoshelevu wa chakula.