Wakulima wajihusisha na kilimo mseto ili kukabili mabadioliko ya tabia ya nchi

  • | West TV
    137 views
    Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, mavuno yamekua yakipungua kila msimu katika kaunti ya Busia, hali hii ikiifanya kaunti hiyo kuorodheshwa miongoni mwa kaunti masikini nchini. Katika muda wa miaka mitano sasa wakulima kaunti hiyo ya Busia wamekua wakikumbatia kilimo cha kustahimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na maisha ya wengi yameonekana kubadilika.