Wakulima walalamikia gharama ya juu ya petroli katika uzalishaji wa chakula kaunti ya Taita Taveta

  • | Citizen TV
    161 views

    Kupanda kwa bei ya bidhaa za petroli kutokana na nyongeza ya ushuru kutoka 8% hadi 16% , wakulima wanaotumia petroli kunyunyizia mashamba yao maji wanasema kupanda kwangharama ya petroli kunaathiri uzalishaji wa vyakula. Akizungumza eneo la Taveta , mwenyekiti wa shirika la wakulima eneo hilo, Daudi Mbele, amesema kuwa wakulima wengi hutumia mafuta na gesi kuzalisha chakula na hivyo wameathirika na nyongeza ya bei ya mafuta. Baadhi wamelazimika kusitisha kilimo na kujitosa kwenye shughuli zingine za kibiashara ili kukidhi mahitaji ya familia zao.