Wakulima wote walioathirika kwenye sakata ya mbolea ghushi kufidiwa na serikali

  • | KBC Video
    32 views

    Hatibu wa serikali Isaac Mwaura amesisitiza kuwa wakulima walionunua mbolea ya kiwango cha chini watafidiwa wote. Akizungumza jijini Mombasa, Mwaura pia alithibitisha kuwa mbolea hiyo iliyosambazwa na kampuni ya KEL Chemicals ilikuwa ya viwango vya chini na hatua itachukuliwa dhidi ya wasambazaji na maafisa wa shirika la humu nchini la kukadiria ubora wa bidhaa KEBS. Maafisa wanane wa ngazi za juu katika shirika la KEBS tayari wamesimamishwa kazi kuhusiana na kutolewa kwa uidhinisaji na nembo za ubora kwa kampuni mbili zilizohusishwa na mbolea hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News