Wakulima zaidi wanakuza parachichi aina ya hass

  • | Citizen TV
    683 views

    Wakulima zaidi katika eneo la Gatundu wanajihusisha na kilimo cha parachichi aina ya hass kutokana na thamani yake katika masoko ya nje. Aidha kilimo hiki kimewavutia wakubwa na wadogo katika jamii, ambao sasa wanajizatiti kutumia mbinu rahisi kufanikisha kilimo chao. Katika makala ya Kilimo Biashara, tunaangazia naibu chifu mmoja Kiambu aliye na boma lililozingirwa na mamia ya miti ya parachichi.