- 824 viewsDuration: 3:16Wakurugenzi wanne wa Nairobi Hospital akiwemo mwenyekiti wa bodi Dkt. Barcley Onyambu wameandikisha taarifa katika makao makuu ya idara ya upelelezi DCI huku sakata ya usimamizi wa hospitali hiyo ikiendelea. Haya yanajiri huku usimamizi wa hospitali ya Nairobi Hospital ukiandaa mkutano wa dharura, ili kuangazia utata unaoendelea kati ya maafisa wakuu wa hospitali hiyo na rais William Ruto.