Wakuu wa usalama waungana na wana bodaboda katika hamasisho la usalama Garissa

  • | Citizen TV
    148 views

    Katika juhudi za kukabiliana na visa vya utovu wa usalama kaunti ya Garissa,kikao maalum kiliandaliwa kati ya maafisa wa usalama na wahudumu wa bodaboda. Mkutano huu ulioandaliwa na shirika la kijamii la Kesho Alliance unalenga kuhamasisha vijana kuhusiana na umuhimu wa kudumisha usalama na kujiepusha na makundi potofu. Kamanda wa polisi James Ng'etich anasema moja wapo wa mikakati ni kuwasajili wahudumu hao kwenye makundi ili kurahisisha utambulisho wao.