Wakuu wa vyama vya wafanyakazi wakerwa na matamshi ya Rais Macron

  • | VOA Swahili
    493 views
    Wakuu wa vyama vya wafanyakazi Ufaransa wamesema hawajaridhishwa kabisa na matamshi ya Rais Macron na wametangaza siku nyingine ya maandamano na migomo, Alhamisi kote nchini. Rais Macron hata hivyo ameeleza kuwa mpango wa mfumo wa malipo ya uzeeni uanze kutekelezwa ifikapo mwisho wa mwaka 2023. Ungana na mwandishi wetu akikuletea ripoti kamili kuhusu utekelezaji wa mfumo huo ikiwemo umri wa kustaafu kuwa ni miaka 64. Endelea kusikiliza... #wafanyakazi #vyama #ufaransa #rais #emmanuelmacron #mfumo #malipoyauzeeni #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.