Walaghai watumia hofu iliopo ya corona kutengeneza dawa bandia

  • | BBC Swahili
    Hofu ya kutojua kitakachotokea kwasababu ya janga la corona imetetoa fursa muruwa kwa walanguzi kutengeneza dawa zao ghushi. Kulingana na Shirika la Afya Dunia (WHO) hadi kufikia sasa hakuna dawa wala chanjo ya ya corona lakini hilo bado halijakuwa sababu ya watu kutojitangaza kwamba wamepata dawa. BBC Africa Eye na mwandishi wa habari za uchunguzi Ghana Anas Aremeyaw Anas wamekuwa wakichunguza mauzo ya dawa bandia inayodaiwa kutibu virusi vya corona na kile mamlaka inachofanya kusitisha ulaghai huu.