Walemavu wa Tanzania wanaolazimishwa kuwa omba omba Kenya -BBC AFRICA EYE

  • | BBC Swahili
    1,422 views
    Walanguzi wa binadamu wanaziwinda familia za watoto walemavu katika maeneo ya mashambani mwa Tanzania. Wanawashawishi kwa ahadi za maisha bora. Watoto hao husafirishwa mamia ya kilomita na kulazimishwa kuwa omba-omba mitaani katika nchi jirani ya Kenya, mara nyingi kwa miaka mingi. Mawasiliano yote na familia zao hukatishwa BBC Africa Eye ilijificha ili kuwafichua walanguzi wanaofanya biashara hii ya faida kubwa na kuwasaidia baadhi ya wahasiriwa kuepuka maisha ya utumwa mamboleo. #BBCAfricaEye #kenya #tanzania