alimu katika Kaunti za Bungoma na Busia wamelalamikia huduma za matibabu kupitia bima ya afya ya SHA, huku wakitoa makataa ya wiki moja kwa serikali kufafanua zaidi hali halisi ya Bima hiyo la sivyo wataandamana.
Wakizungumza baada ya kuzuru baadhi ya vituo vya afya mjini Bungoma vilivyoidhinishwa kuhudumia walimu, wamesema kuwa bima hiyo haishughulikii matakwa yao kama walivyokubaliana na serikali. Wanasema kuwa iwapo bima hiyo haitatekeleza huduma ipasavyo, itakuwa bora warejeshwe kwenye bima ya awali ambayo ilikuwa inawafaa.