Walimu wa kike wapewa mafunzo Trans-Nzoia kukabiliana na maswala yanayochangia afya ya akili

  • | Citizen TV
    90 views

    Muungano wa walimu wa kike katika kaunti ya Trans-Nzoia umeanzisha mafunzo ya kukabiliana na maswala yanayochangia afya ya akili miongoni mwa walimu. Ripoti kutoka tume ya walimu - TSC - inaonyesha kuwa walimu 16 mwaka huu walijitia kitanzi kutokana na msongo wa mawazo.