Viongozi wa muungano wa walimu KUPPET tawi ya Turkana wamejitokeza kufanya maandamano wakilalamikia serikali ya kitaifa kwa kudinda kushughulikia matakwa yao..
Wakizungumza mjini Lodwar, Walimu hao wanasema bima ya afya ya matibabu ya SHA haiwashughulikii kila wanapoenda hospitalini kwa matibabu, licha ya kutozwa fedha kwenye mshahara. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa KUPPET Michael Ejikon, serikali imeshindwa kuajiri walimu wa sekondari msingi JSS 44,000 jinsi walivyokubaliana na sasa bado walimu hao wanahudumu kupitia mkataba wa kandarasi.