- 344 viewsDuration: 1:53Walimu wa shule za Sekondari Msingi kaunti ya Lamu wamefanya maandamano kushinikiza serikali kuwapa ajira ya kudumu. Walimu hao wanasema wanahuzunishwa wanapoona baadhi ya wanasiasa wakitumia mamillioni ya fedha kwa usafiri huku walimu wakilipwa mshahara finyu. Kwenye maandamano yaliyofanyika huko Mpeketoni walimu hao aidha wamelalamikia ukosefu wa vifaa vya kuwasomesha wanafunzi huku wakitaka kujisimamia kama walimu wa sekondari msingi badala ya kutegemea wakuu wa shule za msingi.