- 257 viewsDuration: 1:55Huyu hayo yakijiri Walimu wa sekondari msingi kutoka kaunti ya Tana River wamefanya maandamano mjini Hola kushinikiza tume ya kuajiri walimu TSC kuwapa ajira ya kudumu. Walimu hao wanasisitiza mazingira wanaofanyia kazi ni magumu ikilinganishwa na mshahara wa shilingi 17000 wanayopewa wakisema hazitoshi kukidhi mahitaji yao na familia zao. Wanasema hali hii imepelekea walimu wengi kukumbwa na msongo wa mawazo kutokana na hali ngumu ya maisha huku wengine wakijipata kwenye madeni.