- 448 viewsDuration: 2:13Walimu wa shule za sekondari msingi (JSS) katika Kaunti ya Kwale wameendelea kushinikiza serikali kuwapa uhuru kamili wa kujisimamia badala ya kuendelea kuwa chini ya shule za msingi. Viongozi wa vyama vya walimu vya KUPPET na KEJUSTA wameibua masuala yanayoathiri shule hizo, yakiwemo ukosefu wa uhuru wa kiutawala, miundombinu duni, ukosefu wa mwongozo wazi wa kupandishwa vyeo kwa walimu na kuendelea kwa kandarasi ya muda ya maelfu ya walimu wanagenzi .