Walimu wakuu wataka mfumo wa ufadhili wa elimu ukarabatiwe

  • | Citizen TV
    133 views

    Zaidi ya walimu wakuu 9,000 waliokongamana wametaka mfumo wa kufadhili masomo kufanyiwa marekebisho wakisema shule nyingi zimeshindwa kukidhi mahitaji kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na mfumko wa bei kupanda kwa asilimia 45. Walimu wakuu pia wanaitaka serikali kuu kuwasilisha mgao wa shule mapema wakisema unachangia kwa walimu wakuu kuwatoza wanafunzi ada zaidi shuleni