Walimu watano wanazuiliwa na polisi Nyamira baada ya kumcharaza mwanafunzi viboko 107

  • | Citizen TV
    3,957 views

    Maafisa wa polisi kutoka eneo la Manga, eneo bunge la Borabu katika kaunti ya Nyamira wamewatia mbaroni walimu 5 kutoka shule ya msingi ya Riang'ombe. kati ya waliotiwa mbaroni ni pamoja na mwalimu mkuu na naibu mwalimu mkuu. hii ni baada ya mwanafunzi wa gredi ya 4 kuchapwa na kuumizwa vibaya na mwalimu katika shule hiyo. mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 9 anaripotiwa kwenda kwa mwalimu mmoja kuripoti kuwa shati lake lilikuwa limeibiwa, kabla ya mwalimu huyo kuwaamuru wanafunzi wa darasa la nane kumshika mtoto huyo, na kumpiga viboko 107 vilivyomwacha na majeraha mabaya makalioni.Mwalimu huyo Jackson Marucha anaripotiwa kuwa mafichoni kwani tangu Alhamisi hajafika shuleni.