Walimu watarajiwa wa shule za upili za awali (JSS) kaunti ya Kericho wapanga kufanya maandamano

  • | K24 Video
    43 views

    Walimu watarajiwa wa shule za upili za awali (JSS) kaunti ya Kericho watafanya maandamano ya wiki tatu wakitaka kupewa ajira ya kudumu na tume ya kuajiri walimu (TSC). Vile vile mgogoro huo ulishuhudiwa katika kaunti ya Narok huku walimu wakitishia kuwa masomo yatalemazwa mwaka ujao endapo serikali haitashughulikia maslahi yao.Kaunti ya Makueni imekuwa na taswira kama hiyo huku walimu wakiapa kuwa hawatatia saini mkataba ambao haujarekebishwa.