Walio na gredi mbovu za ulipaji mikopo ya hazina ya hasla hawatapokea mikopo mingine ya serikali.

  • | K24 Video
    9 views

    Wakenya milioni ishirini na tano ambao wamekopa shilingi bilioni sitini na mbili nukta nane katika hazina ya hasla, wote wameorodheshwa katika gredi tisa tofauti kuonyesha uwezo wao wa kulipa mikopo huku walio na uwezo wa chini kabisa wakizuiliwa kupata mikopo mingine ya hazina serikali kama vile ya uwezo na ya vijana. Kulingana na katibu mkuu wa biashara na vyama vidogo vidogo vya ushirika susan mange'eni, ambao wameshindwa kulipa madeni watapunguziwa viwango vya mikopo wanayoweza kupata ila hawataorodheshwa katika CRB.