Walio na stakabadhi feki watakiwa kuondoka serikalini

  • | Citizen TV
    7,527 views

    Zaidi ya wafanyakazi elfu mbili wa sekta ya umma waliopatikana na dosari ya kuwa na vyeti bandia sasa wametakiwa kujiuzulu mara moja na kurejesha mishahara na marupurupu yote. Rais William Ruto ameagiza haya alipofunga rasmi kongamano la kitaifa kuhusu mishahara ambapo pia amewaagiza maafisa wa tume ya ufisadi nchini na idara ya upelelezi kuwa macho na wanaotoa hongo kupata kazi.