Walioharibu mali Embu katika maandamano ya kupinga mswada wa fedha washtakiwa

  • | KBC Video
    12 views

    Kamishna wa kaunti ya Embu Jack Obuo ametangaza msamaha wa wiki mmoja kwa watu wanaomiliki mali iliyoibwa wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024. Wakati wa maandamano hayo afisi za halmashauri ya ukusanyaji ushuru humu nchini katika kaunti ya Embu ziliporwa na mali kuharibiwa.Obuo alisema kuwa watu 23 wameshtakiwa kuhusiana na visa 16 vya uharibifu wa mali katika kaunti hiyo .Aidha Obuo alisema kuwa maafisa wa usalama wanawasaka watu zaidi waliotekeleza uhalifu huo .Kuhusiana na vileo gushi na pombe haramu , Obuo alisema kuwa kamati ya usalama haitalegeza kamba katika vita dhidi ya biashara hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive