Waliokopa kwenye hazina ya Hustler fund wakosa kulipa madeni yao

  • | Citizen TV
    3,728 views

    Serikali sasa inasema italazimika kufutilia mbali deni la shilingi bilioni sita lililochukuliwa kutoka kwa hazina ya hustler kwani waliopewa mikopo hawajalipa. Katibu wa idara ya biashara ndogo Susan Mang'eni akisema juhudi za kuwatafuta waliotoroka na mikopo zimegonga mwamba. Sasa serikali inawataka wabunge kupitisha shilingi bilioni tano zaidi kwenye bajeti ya mwaka huu kufadhili hazina hiyo.