Walionufaika na Bajeti I Wizara ya elimu yatengewa mgao mkubwa zaidi wa fedha

  • | KBC Video
    21 views

    Walimu wanaotafuta ajiira ndiyo watakaonufaika zaidi na bajeti iliyowasilishwa bungeni leo baada ya serikali kutangaza kwamba itawaajiri walimu 20,000 wakati wa kipindi cha kifedha cha mwaka huu. Hali kadhalika wanafunzi wa shule za sekondari msingi wanatarajiwa kupata vifaa bora vya masomo kutokana na mgao wa shilingi bilioni 628.6 zilizotengewa sekta ya elimu kwenye bajeti hiyo. Na ikiwa wewe ni mkulima, utanufaika pakubwa baada ya serikali kutangaza ruzuku ya mbolea iliyotengewa shilingi bilioni 5 kwenye bajeti. Hatua hiyo inanuiwa kupunguza gharama ya uzalishaji chakula na hatimaye kupunguza bei ya bidhaa za vyakula.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #budget2023