Wamarekani waelekea vituo vya kupiga kura kuamua nani adhibiti bunge

  • | VOA Swahili
    1,604 views
    Wapiga kura Marekani wanaelekea kwenye debe kuamua nani atakayechukua udhibiti wa bunge kati ya Wademokrat na Warepublikan katika uchaguzi wa katikati ya muhula. - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba dunia itaangamia kutokana na mabadiliko ya hewa iwapo hatua hazitachukuliwa. - Maombi maalum yamefanyika kwa ajili ya watu waliofariki kutokana na ajali ya ndege Bukoba, Tanzania. - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.