Wana-ODM wamuombea Raila kuhusu uchaguzi wa AUC

  • | Citizen TV
    2,206 views

    Wajumbe wa chama cha ODM wanafanya mkutano wa maombi maalum kwa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, siku nne kabla ya uchaguzi wa uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika kuandaliwa Raila anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambako uchaguzi huo utaandaliwa siku ya jumamosi. Mkutano huo wa Bomas unanuiwa kuimarisha maombi kwa ushindi wa Odinga anayewania kiti hicho. Raila anawania wadhifa huu dhidi ya Mohamoud Youssouf wa Djibouti na Richard Randriamandrato wa Madagascar. Endapo atapata ushindi, basi Odinga atamrithi Moussa Faki anayekamilisha muda wake