Wanafunzi 100 wahitimu mafunzo ya kompyuta kwenye mradi wa huduma za kitaifa za maktaba nchini

  • | Citizen TV
    220 views

    Wanafunzi 100 wamehitimu katika mafunzo ya kompyuta kwenye mradi wa huduma za kitaifa za maktaba nchini. Masomo hayo yanayotolewa bila malipo kwa vijana katika kaunti ya Taita Taveta yananuiwa kuwapa vijana ujuzi wa kuwawezesha kubuni mbinu za kisasa za kujipatia ajira. Naibu msimamizi wa maktaba ya Voi Benerd Kilaghai amesema kuwa idadi kubwa ya vijana hawajui kusoma na kuandika kikamilifu na kuwa mafunzo hayo ya kompyuta yatawawezesha vijana kuwa na ujuzi wa kidigitali. Mradi huo unalenga kutoa mafunzo kwa zaidi ya vijana 2500 kufikia mwisho wa mwaka huu.