Wanafunzi 11 wa chuo kikuu cha Kenyatta wafariki

  • | Citizen TV
    5,546 views

    Wanafunzi 11 wa chuo kikuu cha Kenyatta wameaga dunia huku wengine 46 wakipata majeraha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Maungu huko Voi jana usiku. Mipango ya kusafirisha maiti ya wanafunzi hao hadi hospitali ya rufaa ya chuo hicho inaendelea...Ajali hiyo ilitokea pale basi la chuo lilipogongana na lori katika eneo hilo la Maungu kwenye barabara kuu ya Nairobi kueleka Mombasa...Waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali tofauti za eneo hilo huku wengine wakisafirishwa kwa ndege hadi hapa jijini nairobi kwa matibabu maalum .