Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi 16 wafariki katika moto Utumishi Academy, Gilgil

  • | Citizen TV
    736 views
    Tunaanza taarifa zetu na tanzia kufuatia mkasa wa moto uliotokea katika shule ya wasichana ya Utumishi Academy eneo la Gilgil, kaunti ya Nakuru, ambapo hadi alasiri ya leo maafisa wa upelelezi walikuwa wameondoa miili ya wanafunzi kumi na sita waliofariki katika ajali hiyo. Zoezi la uokoaji na uchunguzi lililoanza jioni limeendelea huku wazazi wengi wakiwa bado hawajapata taarifa kamili kuhusu hatma ya watoto wao. Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen pamoja na Waziri wa Elimu Migos Ogamba wameongoza ujumbe wa serikali na kuahidi kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha mkasa huo. Ben Kirui yuko Gilgil na anaendelea kufuatilia hali hiyo iliyojaa majonzi, hasira na hofu miongoni mwa jamii iliyoathirika.