Wanafunzi 99 wa Eregi Girls walazwa hospitalini

  • | Citizen TV
    3,583 views

    Wanafunzi tisini na tisa kutoka shule ya wasichana ya eregi wamelazwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa ambao bado haujatambuliwa. Wasichana hao walianza kuonyesha dalili za kushindwa kutembea na kupooza. Wazazi waliofika shuleni kuwachukua wanao walikatazwa kuwaona au kwenda nao nyumbani kutokana na hofu ya ugonjwa huo kusambaa zaidi.