Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi Loruk wakumbwa na hatari baada ya ziwa Baringo kuvunja kingo

  • | Citizen TV
    444 views
    Duration: 3:11
    Mamia ya wanafunzi katika eneo la Loruk, Baringo Kaskazini, wanaishi katika hatari baada ya Ziwa Baringo kuvunja kingo zake. Zaidi ya wanafunzi 250 kutoka Shule ya Loruk wanalazimika kuhatarisha maisha kila wanapoelekea shuleni baada ya barabara ya kuingia katika shule hiyo kukatika. Hali hiyo imewalazimu wazazi kuchangia shilingi 20 kwa kila mwanafunzi ili kulipia usafiri wa boti unaowasafirisha wanafunzi hao kwenda shuleni.