Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi tisa kusalia rumande kufuatia mkasa wa moto Utumishi Academy

  • | Citizen TV
    13,676 views
    Duration: 3:08
    Wanafunzi tisa wanaodaiwa kusababisha vifo vya wanafunzi wenzao kumi na sita kwenye mkasa wa moto katika shule ya upili ya wasichana ya Utumishi Academy, Gilgil, watasalia seli hadi kesho ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la. Upande wa mashtaka umeiomba mahakama kuruhusu wanafunzi hao wazuiliwe kwa siku thelathini ili uchunguzi ukamilishwe. Maafisa wa usalama waliweka doria kali nje na ndani ya mahakama ya Naivasha wakati washukiwa walipowasilishwa mahakamani.