Wanafunzi wa Afrika wadaiwa kukataliwa visa za kwenda kusoma Marekani

  • | VOA Swahili
    89 views
    Wanafunzi kutoka nje ya Marekani wanaotaka kusoma katika taifa hili lazima waombe VISA ya F- 1 kupitia wizara ya mambo ya nje. VISA hiyo inaruhusu wanafunzi kuishi Marekani wakati wanasoma. Ripoti ya Julai 2023 kutoka viongozi wa ushirika wa elimu ya juu iligundua kwamba wanafunzi wa Afrika wanakataliwa VISA hii kwa kiwango kikubwa kuliko wale wanaotoka kwenye mabara mengine. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.