- 57 viewsWanafunzi wa chuo kikuu cha Bomet na wanajamii wanalalamikia ujenzi wa eneo la kutupa taka karibu na chuo hicho na mto wa Nyangores. Wanafunzi hao Wanasema kuwa licha ya kushinikiza serikali ya kaunti ya Bomet kutenge mahali mbadala, ujenzi umeendelea bila jamii kuhusishwa au athari za taka kuzingatiwa. Serikali ya kaunti ilianza kutupa takahapo baada ya jalala la awali lililokuwa karibu na nyumba za bei nafuu kuondolewa. Wakazi sasa wanataka jalala kuhamishwa kwa dharura.