Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Nairobi wapanga mgomo

  • | KBC Video
    37 views

    Viongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi wametishia kufanya maandamano kulalamika kuhusu mfumo mpya wa kufadhili wanafunzi vyuoni. Wanafunzi hao wamewahimiza wenzao katika vyuo vingine kushiriki maandamano hayo ya kitaifa yaliopangiwa kufanyika tarehe-2 mwezi ujao. Kwenye kikao na wana-habari katika bewa kuu la chuo kikuu cha Nairobi, rais wa chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi, Rocha Madzayo alisema wamejaribu kuzungumza na serikali kubadili au kutupilia mbali mfumo huo wa ufadhili lakini juhudi zao zimegonga mwamba.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive