Wanafunzi wa kike kaunti ya Busia wapata baiskeli kuwasaidia kwa safari kwenda shuleni

  • | Citizen TV
    501 views

    Wanafunzi kutoka katika familia zisizojiweza na ambao hulazimika kutembea mwendo mrefu kufika shuleni Busia, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupewa baiskeli ili kuwawezesha kufika shuleni bila matatizo. Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi wanaotoka mbali na ambao wazazi wao hawawezi kumudu gharama ya usafiri kuelekea shuleni imeathiri pakubwa elimu ya wanafunzi wa kike wa shule za kutwa, huku baadhi yao wakilazimika kuacha shule.