- 551 viewsDuration: 3:04Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanaafikia ndoto zao maishani. Wito huu umetolewa baada ya kundi la wasichana wa Shule ya Upili ya Lenana kaunti ya Trans Nzoia kurejea nchini kutoka Uingereza, walikokwenda kupata mwongozo wa uongozi bora. Wanafunzi hao wanasema safari hiyo imekuwa yenye manufaa makubwa kwani mbali na kujifunza mbinu za uongozi, pia imewasaidia kuelewa umuhimu wa maadili mema katika jamii.