- 3,435 viewsWanafunzi wanane wa shule ya upili ya wasichana ya Utumishi ya gilgil kaunti ya nakuru wamekamatwa wakihusishwa na mkasa wa moto ulitokea usiku wa Jumatano na kusababisha maafa ya wanafunzi kumi na sita. Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo huku uchunguzi wa kina ukiendelea. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa njama ya kuteketeza bweni ilipangwa na baadhi ya wanafunzi ambao walionyesha kutoridhishwa na usimamizi wa shule hiyo hasa mwalimu mkuu