- 8,781 viewsDuration: 1:06Wanafunzi hawa walionyesha ujasiri mkubwa baada ya dereva wao kupoteza fahamu akiwa anaendesha basi huko Mississippi, Marekani. Badala ya kupata hofu na kuogopa, mmoja wao alichukua usukani na kusimamisha basi salama huku wengine wakipiga simu kuomba msaada na kutoa huduma ya kwanza kwa dereva, Leah Taylor (46), aliyepatwa na shambulio la pumu. Dereva huyo alipona kabisa na kuwashukuru wanafunzi hao kwa kuokoa “maisha yake na ya kila mtu aliyekuwa ndani ya basi hilo.” #bbcswahili #marekani #UsalamaBarabarani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw