Wanafunzi washiriki tamasha la kupendeza la Cape Town Carnival

  • | VOA Swahili
    29 views
    Raia mmoja wa Afrika Kusini ambaye alipitia uonevu, akiwa katika shule ya upili, anawaenzi wanafunzi wake, wa dansi, wanaoshiriki katika Tamasha la kupendeza la Cape Town Carnival. UNICEF inasema utafiti wa hivi karibuni uligundua wanafunzi vijana milioni 10 katika eneo la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, wanapitia uonevu, na madhara yanaweza kuendelea hadi utu uzima. Mwandishi wa VOA, Vicky Stark, anaarifu zaidi, na BMJ Muriithi anasimulia ripoti yake. #afrikakusini #uonevu #shuleyaupili #wanafunzi #dansi #tamasha #capetowncarnival #unicef #voa #voaswahili