Wanafunzi wasimulia yaliyojiri wakati wa mkasa shuleni Kakamega

  • | Citizen TV
    Ni mengi yamesemwa kuhusiana na yaliyojiri katika shule ya msingi ya kakamega na kusababisha mkurupuko uliosababisha vifo vya wanafunzi 15. Huku waathiriwa wote wakiwa wamezikwa, wachunguzi wanasalia na maswali kwa wanafunzi walionusurika angalau kupata majibu kuhusiana na kilichojiri siku ya mkasa. Na kama raquel muigai anavyotuarifu, maisha yamebadilika kwa wazazi waliowapoteza watoto wao na kwa wale pia wamesalia na majeraha kutokana na kile kinaaminika kuwa mchezo uliobadilika na kuwa mauti