Wanahabari waandamana sehemu mbalimbali nchini

  • | Citizen TV
    835 views

    Waandishi wa habari walifanya maandamano katika sehemu mbalimbali nchini ili kushinikiza uwajibikaji wa serikali kuhusiana na visa vya kukandamiza uhuru wa uanahabari. Katika kaunti ya Nairobi, wanndishi walifika hadi makao ya polisi ambapo waliwasilisha malalamishi yao kwa msemaji wa polisi Resila Onyango. Vile vile, waandishi kutoka sehemu zingine humu nchini pia walizungumzia ukandamizaji ya uhuru wa kujieleza.